Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih Dauda: Madhaifu makubwa ya Simba yapo kwa Inonga

Shaffih X Inongaaaa Shaffih Dauda: Madhaifu makubwa ya Simba yapo kwa Inonga

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati joto la Dabi ya vigogo wa Kariakoo Simba vs Yanga likizidi kupanda kuelekea Novemba 5.

Wadau mbalimbali wameendelea kuchambua ubora na udhaifu wa vikosi vya Timu hizo na hapa mchambuzi wa Michezo kutoka Clouds FM, Shaffih Dauda anataja udhaifu wa Simba SC.

Akizungumza Shaffih anasema;

"Madhaifu makubwa ya Simba yapo kwa Henock Inonga, ni mchezaji anayependa kukokota mpira na kujaribu kupiga chenga ambazo mara nyingi huwa hazina faida kwa klabu kwa maana ya kimbinu."

"Huwa anafanya vitu vingi ambavyo binafsi sioni kama vina faida badala yake vinaiweka klabu kwenye nafasi ngumu endapo ikitokea wamepoteza mpira, ukiangalia Che Malone anajaribu kuziba makosa yanayofanywa na Inonga lakini kwa kuwa Inonga anafanya vitu vinavyopendwa na watu wengi basi huwa inamfanya asiangaliwe sawa lakini ni makosa ambayo hayatakiwi kwa nafasi yake."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: