Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki awachana viongozi wa Simba SC "Hawajui mpira"

Simba Mangunguuuuuuu Shabiki awachana viongozi wa Simba SC

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, Yusuph Mwenda maarufu kama Mzee Mwenda anasema kuwa viongozi wengi wa timu hapa nchini hawaujui mpira, ambapo kawatolea mfano Viongozi wa klabu ya Simba SC.

Mwenda amesema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari kufuatia usajili wa kipa mpya wa Simba raia wa Morocco, Ayoub Lakred baada ya yule aliyesajiliwa awali, Jefferson Luis kurudi kwao kwa kukosa vigezo vya kucheza Ligi Kuu ya Tanzania.

“Kama hii juzi unamuacha Baleke nje, unamchezesha Bocco dakika 70 unaujua mpira? Kuna maelekezo huko nje ambayo yanatuharibia soka. Kocha anataka huyu mtu wangu acheze, hawa ndio wanatuharibia mpira, hawa ndio wanaovurunda, wawaachie wanaojua.

“Kocha ndiye alisema tukamletee wachezaji, wa nini sasa kama hawacheji? Viongozi wengi waliojichomeka kwenye uongozi wa soka kwenye hizi timu hawaujui mpira ni tofauti na wenzetu kule Ulaya. Mtu hajawahi kucheza mpira wala kuusoma lakini anapewa madaraka, anapokurupuka ndiyo inakwenda kuleta shida.

“Simba tulimsajili kipa wa daraja la nne, wakaja kusema heti ameumia, hakuna kitu kama hicho, ule ni ubabaishaji, mtu alikwenda tu hajui, sababu waliokabidhiwa lile rungu si wanamichezo. Walikwenda tu wakaburuta baadaye wakaigeuza stori," amesema Mwenda.

Nini maoni yako?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: