Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba awavaa Robertinho, Mgunda

Simba 0110 Shabiki Simba awavaa Robertinho, Mgunda

Fri, 5 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Simba, Yusuph Mwenda ameonyesha kuchukizwa na kitendo cha kocha wa timu hiyo, Robertinho kupanga kikosi cha pili katika mechi yao dhidi ya Namungo hali iliyosababisha kutoa sare.

Mwenda amesema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa Ligi katika Dimba la Majaliwa.

"Sisi Simba hatutaki kujaribu kwenye mechi zetu, tungeshinda kwa Namungo jana tulikuwa tunawapa pressure Yanga wakiteleza tunakaa. Sasa makocha na viongozi walituaminisha vipi kwamba ubingwa bado tunaupambania.

"Kocha Mgunda anarahisha tu kuongea lakini tunaoumia ni sisi, yeye pale analipwa mshahara na posho tu, ila wenye timu ni sisi. Wameanzisha wachezaji ambao hawawezi kutusaidia kushinda," amesema Mwenda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: