Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba: Benchikha hana uwezo

Benchikha Mapinduzi.jpeg Shabiki Simba: Benchikha hana uwezo

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa kocha wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha hana uwezo wa kuifundisha timu hiyo kwani imekuwa ikipoteza matokeo kwenye mechi za muhimu ikiwa ni miongoni mwa timu inayowania ubingwa.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

"Ni fedheha kwa Klabu ya Simba kufungwa na Prisons, tumetoka kushinda bao 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy, tunakuja kufungwa na Prisons tena baada ya kadi nyekundu jamaa wakata pungufu. Alama tatu ambazo tumezipoteza ni za muhimu sana, naona tunadanganyana.

"Nashindwa kujua uwezo wa Benchikha, sijui wachezaji wameshindwa kuingia kwenye mfumo wake au yeye ameshindwa kuingia kwenye mfumo wa wachezaji. Mpaka sasa hana kikosi cha kwanza, akiamka anampa yeyote tu akacheze nafasi yoyote," amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: