Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba: Ahemd Ally aache mdomo

Ahmed Ally LEO Shabiki Simba: Ahemd Ally aache mdomo

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amemtaka Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Ahmed Ally kuacha kuwasema wachezaji wa timu nyingine badala yake kuizungumzia timu yake.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Msema ji wetu aache mdomo, amemsema sana Mbangula kumbe anamhamasiha mpinzani, anapata motivation mwisho wa siku anatufunga bao mbili na tunapoteza alama tatu.

“Msemaji wetu anakuwa motivational speaker wa timu pinzani, anawahamasisha wapinzani mwisho wa siku tunafungwa, aache hizo mambo aongelee soka na timu yake, aache kuwasema watu.

“Amewasema Yanga tukala tano, amewasema Azam FC wee mwisho wa siku wakatupiga, tumechomoa tena dakika za mwisho roho mkononi, Msemaji ajitathmini,” amesema Mchome

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: