Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki: Lakred hana ubora, akidaka natazama mpira na Panadol

Lakred Ayoub Trsns Shabiki: Lakred hana ubora, akidaka natazama mpira na Panadol

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki wa Klabu ya Simba, Nabii Meja anasema kuwa siku akiwa nadaka golini kipa mpya wa Simba SC, Ayoub Lakred yeye huwa anaangalia mpira huku akiwa ana Panadol pembeni ili kupoza maumivu.

Meja amesema hayo akidai kuwa Lakred ambaye ni raia wa Morocco hana ubora wa kudakia Simba lakini anashangaa amesajiliwaje kwenye kikosi hicho na kupangwa kucheza.

“Nafasi ambazo wanampa huyu kipa wa sasa wa Simba, Ayoub huwa ninaangalia huku nikiwa na Panadol. Yani ninaumia, inawezekana vipi benchi zima la ufundi, timu nzima ya Simba Sc wanashinda kuona kwamba huyu kipa ana mapungufu kuliko mapungufu yenyewe?

“Ile mipira hata mtoto wangu anadaka. Tuwe serious, yule kipa ana uwezo mdogo sana, hata mashabiki wachukie, viongozi wa Simba wachukie lakini ukweli ni kwamba Ayoub ana uwezo mdogo sana wa kudaka, yani kudaka kuzuia ana uwezo mdogo.

“Jana yalipigwa mashuti machache na Coastal Union kwa sababu tu walikuwa hawawezi kuingia sana kwenye boksi la Simba. Walipiga mashuti mawili matatu lakini hakuweza kuyatendea haki, hata namna anavyo-punch mpira unaona kabisa kwamba hana uwezo,” amesema Nabii Meja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: