Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekilojo Chambua aipeleke Young Africans Nusu Fainali

Yanga 1170x650.jpeg Sekilojo Chambua aipeleke Young Africans Nusu Fainali

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: Dar24

Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Young Africans, Sekilojo Chambua amesema timu hiyo ina nafasi ya kuingia Nusu Fainali kwa kuifunga Mamelodi Sundowns nyumbani kwao.

Young Africans wapo nchini Afrika Kusini, ambapo wao wataanza kushuka kwenye dimba la Loftus Versfeld kucheza dhidi ya Mamelodi Sundowns ya huko, mchezo utaopigwa saa 3:00 usiku wa saa za Afrika Mashariki.

Chambua aliyetamba na Young Africans mwanzoni mwa miaka ya 1990 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000, amesema timu hiyo ina nafasi ya kusonga mbele kama watacheza kwa nidhamu kama walivyofanya katika mechi ya kwanza wiki moja iliyopita.

“Kwenye mechi hizi muhimu ni kumuheshimu mpinzani wako na kutumia nafasi chache zinazopatikana. Kama Young Africans watafanya hivi nina imani wataingia Nusu Fainali” amesema kiungo huyo wa zamani wa Tukuyu Stars ya Mbeya.

Amesema Young Africans wana timu imara na kurejea kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi kama Pacome Zouzoua na Khalid Aucho kutaongeza hali ya kujamini kwa timu.

“Mechi ya Dar es Salaam kidogo ilinipa hofu baada ya kikosi kutoka. Lakini walicheza kwa nidhamu na matokeo ya mechi ile yamefanya mchezo huu wa marudiano kuwa wazi kwa timu zote mbili,” amesema Chambua.

Chanzo: Dar24
Related Articles: