Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sawadogo, Banda waipasua Simba SC

Banda Sawadogo Sawadogo, Banda

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba imemaliza msimu wa 2022-2023, bila taji lolote na kinachoendelea kwa sasa ni vikao vya mara kwa mara kwa mabosi wa klabu hiyo kwa lengo la kupanga mikakati ya kusuka kikosi kikali kwa msimu ujao, huku ikielezwa kiungo Ismael Sawadogo na winga Peter Banda wakiwagawa mabosi hao.

Mbali na Banda na Sawadogo kuwagawa mabosi hao, lakini baadhi ya wachezaji wengine wa kikosi hicho kwa sasa wanafanyiwa mipango ya kupeleka nje ya nchi ikiwa ni utekelezaji wa mikataba mpya wa makubaliano ambayo klabu hiyo iliingia na West Armenia FC.

Mkataba huo uliosainiwa katikati ya wiki iliyopita, Simba na West Armenia zimekubaliana kuwa na ushirikiano wa pamoja unaotoa fursa kwa kuuziana wachezaji, maendeleo ya ufundi, soka la vijana na maendeleo ya soka.

Ipo hivi. Mabosi wa Simba wamekuwa kwenye vikao mfululizo vya Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekiti, Salim Abdallah 'Try Again', huku mada kubwa ikiwa ni usajili wa wachezaji wapya sambamba na wanaoachwa kutokana na kushindwa kufanya vizuri.

Hata hivyo vigogo hao waligawanyika kwenye ishu ya kuwapiga chini Banda anayetakiwa na Azam ambaye amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja, sambamba na kiungo Mburkina Faso, Ismael Sawadogo, huku baadhi ya wachezaji wakipigiwa hesabu za kupelekwa West Armenia.

Sawadogo na Banda wote bado wana mkataba wa mwaka mmoja na Simba ambapo kwa Sawadogo wako tayari kuuvunja lakini inaonekana watatakiwa kumlipa pesa ndefu huku kwa Banda viongozi wakigawanyika kuhusu kumuacha.

Wapo wanaoamini Banda ana kipaji kikubwa na umri wake unamruhusu kuendelea kucheza Simba wakiwa na matumaini ya winga huyo kufanya vizuri kwenye misimu ijayo lakini pia wapo wanaodhani ni muda wake kuondoka kwani ameshindwa kuonyesha muendelezo wa kiwango chake katika muda aliokaa Simba na amekuwa na majeraha ya mara kwa mara.

Hata hivyo, uongozi wa Simba upo tayari kupokea ofa ya timu yeyote itakayohitaji huduma ya wawili hao kwa mkataba wa mkopo ama kununuliwa jumla.

Ripoti zinaeleza Azam ni miongoni mwa timu zinazovutiwa kumsajili Banda na uongozi wa timu hiyo ukirudi Dar es Salaam kutokea Tanga ulikoenda kwenye mechi ya fainali ya kombe la TFF (ASFC), huenda ukafungua majadiliano rasmi na Simba juu ya winga huyo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: