Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanga: Tatizo la Simba ni Mo Dewji, aondoke!

Sanga Dewji Mdsg Sanga: Tatizo la Simba ni Mo Dewji na viongozi

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku moja baada ya Mwanachana na Shabiki wa Simba SC Ally Mikoi ‘Kisugu’ kumtaka Mbunge wa Makete Festo Sanga kuacha kuizungumzia Simba SC vibaya, Mbunge huyo ameibuka na kumjibu Kisugu.

Mbunge Sanga amesema haishambulii Simba SC kama inavyozemwa na wengi na kuongeza ni mapenzi yake dhidi ya timu hiyo.

“Mwenendo wa Klabu yetu ya Simba ambayo ninaishabikia sio mzuri, kwa heshima, kwa hadhi, kwa umri na kwa namna ambavyo tunaijua na inavyoenda kwa sasa hairidhishi na mwenendo huu ni matokeo ya vitu flani.

“Kwanza ni aina ya uongozi unavyoendesha mambo yake na pili ni aina ya uwekezaji na mwekezaji mwenyewe anavyo-behave ndani ya klabu. Kwenye Taifa letu kuna Yanga na Simba, zinatambulisha taifa letu kisoka, zote zimeamua kutoka kwenye community based club kwenda kwenye mfumo wa kampuni.

“Wenzetu Yanga wanafanya mchakato wa mabadiliko ambao na sisi Simba tunafanya, lakini sisi Simba tuna ukata, mwekezaji haeleweki, akijitokeza kwenye media anasema timu inampa hasara, kama anakula hasara kuna haja gani ya kuendelea kuikumbatia hiyo timu? Akijitokeza anasema ameinunua timu, sisi tunachojua Simba haijaingia kwenye soko la hisa, hizo hisa zilinunuliwa linin a zilinunuliwa shilingi ngapi?

“Ili tuinusuru Simba lazima kwanza tukubali kuwa timu ina changamoto na mashabiki tuwaambie ukweli. Kuugulia mioyoni sio suluhisho la kutibu matatizo yetu, tuseme ukweli changamoto zipo, timu haina hela, mwekezaji analeta janja janja kwenye klabu yetu ya Simba, kama anapata hasara anaweza akapisha wawekezaji wengine wakaingia na timu ikarudi kwenye hadhi yake," amesema Sanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: