Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido aondoka Simba na rekodi tamu, takwimu zambeba

Snapinsta Saido Saido Ntibazonkiza

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Klabu ya Simba juzi iliachana rasmi na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Mrundi, Saidi Ntibazonkiza 'Saido' baada ya mkataba wake kumalizika huku nyota huyo akiondoka na rekodi tamu tangu alipoanza kucheza Ligi Kuu Bara.

Juzi Simba ilitangaza kuachana na Saido akiwa ni mchezaji wa pili baada awali kumuaga John Bocco, pia wakafuata Shaaban Chilunda, Luis Miquissone na Kennedy Juma.

Nyota huyo kwa mara ya kwanza alitua nchini Oktoba 12, 2020, aliposajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga akitokea Vital'O FC ya kwao Burundi na kukitumikia kikosi hicho kwa misimu miwili kisha kuachana nacho rasmi Julai Mosi, 2022.

Katika misimu miwili aliyoichezea Yanga, alicheza jumla ya michezo 18 ya Ligi Kuu Bara akihusika katika mabao 10 ambapo alifunga saba na kutoa pasi tatu za mabao. Baada ya hapo akajiunga na kikosi cha Geita Gold ambapo alicheza michezo 11 ya Ligi Kuu Bara huku akihusika katika jumla ya mabao 10, alifunga manne na kutoa pasi sita za mabao kiwango ambacho kiliwavutia mabosi wa Simba na kumsajili Desemba 29, 2022.

Kiwango Simba

Usajili wake wa kwenda Simba uliwashtua wadau wengi huku baadhi yao wakionekana kuukosoa kwa kile walichoeleza kiwango chake kushuka ingawa baadaye aliwafunga midomo kutokana na ubora wake.

Msimu wake wa kwanza wa 2022/2023, licha ya kuingia dirisha dogo la Januari alicheza jumla ya michezo 12 ya Ligi Kuu Bara ambapo alihusika katika mabao 19, baada ya kufunga 13 wastani wa bao moja kila mchezo na kuchangia sita huku akiwa kinara kwa upande wa Simba.

Chanzo: Mwananchi
Related Articles: