Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido afunga bao la 201 CAF

Saido Asec.jpeg Saido afunga bao la 201 CAF

Sun, 26 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la Saido Ntibazonkiza ni la kwanza kwake kuifungia Simba katika mashindano ya kimataifa tangu ajiunge nayo mwaka jana.

Ni bao la 139 kwa Simba kufunga katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo awali yalikuwa yakifahamika kama Klabu Bingwa Afrika.

Katika mashindano yote ya klabu Afrika ambayo Simba imeshiriki, bao hilo la Saido Ntibazonkiza ni la 201. Kabla ya hapo Simba ilikuwa imefunga mabao 200.

Mgawanyo wa mabao hayo 201 ya Simba kwenye Mashindano ya Klabu Afrika ni kama ifuatavyo.

Mabao 139 yamefungwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, mabao 42 yamefungwa katika Kombe la Shirikisho Afrika, mabao 17 yamefungwa katika Kombe la CAF, mabao 3 yamefungwa katika Kombe la African Football League

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: