Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido aacha msala kwa Phiri, Luis

Phiri X Jose L Saido aacha msala kwa Phiri, Luis

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba ina siku moja tu za kukaa Dar es Salaam kabla ya Alhamisi Septemba 14, kupaa kwenda Zambia kucheza mechi ya kwanza ya mtoano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya nchini humo itakayopigwa Septemba 16, mwaka huu huku washambuliaji Moses Phiri na Luis Miquissone wakiachiwa shoo nzima.

Ubora waliouonyesha wawili hao katika kipindi hiki cha mapumziko kwenye mechi tatu za kirafiki dhidi ya Kipanga, Cosmopolitan na Ngome ambazo Phiri alifunga mabao mawili na Luis kufunga moja ni kati ya sababu zinazompa jeuri Robertinho na kuanza kupiga hesabu za kuwapa mechi dhidi ya Dyanamos.

Washambuliaji hao hawakuwa kwenye kiwango bora mwanzoni mwa msimu kwani Phiri alikuwa ametoka kuuguza majeraha huku Luis akikosa utimamu wa mchezo (match fitness) kutokana na kukaa muda mwingi bila kucheza lakini sasa wamejipata.

Nafasi yao kuachiwa mechi dhidi ya Dyanamos inazidi kuwa kubwa kwani Simba ipo nusu nusu, kukosa huduma ya mshambuliaji wake hatari wa kikosi cha kwanza Mrundi Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’, aliyeibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu kwa msimu uliopita akitupia mabao 17, kutokana na kubanwa na ratiba ya timu ya taifa lake.

Saido yupo nchini Cameroon na timu yake ya taifa (Burundi), na jana usiku wamecheza mechi mwisho ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2023) dhidi ya Cameroon nakupkea kichapo cha mabao 3-0

Hata hivyo, huenda akakwama kujiunga na timu ndani ya muda tarajiwa jambo ambalo kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amelishtukia na sasa anatafuta mchezaji atakayeziba pengo la Saido kati ya Phiri na Luis.

Saido amekuwa mhimili wa Simba kwenye safu ya ushambuliaji tangu amejiunga na timu hiyo msimu uliopita na msimu huu ameendelea hivyo huku akiungana na Clatous Chama, Kibu Denis na Willy Onana kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Wekundu wa Msimbazi hao.

Hata hivyo, hilo halina shida kwa Simba kwa mujibu wa Robertinho kwani anaamini Phiri na Luis tayari wamekuwa kwenye utayari wa kucheza na wamerejea kwenye viwango vyao. “Simba ina wachezaji wengi, Luis na Phiri ni miongoni mwao na uzuri wanaweza kucheza maeneo tofauti uwanjani. Nafurahi wapo kwenye kiwango bora na nipo tayari kuwatumia kwa mechi zijazo,” alisema Robertinho.

Simba imecheza mechi mbili za mashindano hadi sasa ikiwa ni zile za Ligi ilizoshinda zote, dhidi ya Dodoma Jiji (2-0) ambapo Phiri na Luis waliingia kwa pamoja katika dakika ya 54 ya mchezo huo na Phiri kuifungia Simba bao la pili, sambamba na ule dhidi ya Mtibwa (4-2), walioingia kwa nyakati tofauti katika kipindi cha pili.

Kabla ya kupata majeraha msimu uliopita, Phiri ndiye mchezaji aliyekuwa ameifungia Simba mabao mengi kwa msimu huo akicheka na na nyavu mara 19 akifunga 10 kwenye ligi, matano kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na manne kwenye Kombe la Azam Federation (ASFC).

Kramo hati hati

Staa wa Simba, Muivory Coast, Kramo Aubin huenda akakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kujitonesha majeraha katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ngome na Mwanaspoti imepenyezewa kwamba kama atakuwa na jeraha kubwa basi atapewa mapumziko arudi kwao akajitibu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: