Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu Jobe, Sarr kunyoa rasta

Sarr Jobe Pic Sababu Jobe, Sarr kunyoa rasta

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wengi wanajiuliza kwanini wachezaji wawili wapya wa Simba Babacar Sarr na Pa Omary Jobe wamenyoa rasta kwa wakati mmoja.

Jana picha kutoka mazoezi ya Simba yanayofanyika Mo Arena zilionekana picha za wawili hao wakiwa na mtindo  wa nywele tofauti na jinsi watu walivyowazoea. Wachezaji hao ni maingizo mapya ya dirisha dogo msimu huu.

Jobe ambaye amecheza mechi tano mpaka sasa amefunga mabao mawili na asisti moja huku Sarr akifunga moja tu bila asisti.

Akizungumza na Mwanaspoti Sarr, alisema kunyoa hakuna maana yoyote ila ni maamuzi yake  binafsi ya kutaka kubadilisha muonekano.

"Nimetaka kuwa tofauti na ninavyoonekana wala sio swala kubwa la kuwashangaza kwani lazima mtu abadilike badilike kidogo, pia niko huru sana na huu muonekano mpya."

Jobe alisema wameamua kubadilika yeye na Sarr kwa sababu wamekuwa marafiki kwa sasa hivyo ni makubaliano ya kawaida tu.

"Ulikuwa ni uamuzi wetu tu, tulifikiria kwenda saluni kujiweka sawa, tukaamua tuzinyoe kwa pamoja, hakuna ambaye ametushinikiza ni uamuzi wetu binafsi," alisema Jobe.

Wawili hawa hawana historia ya kucheza pamoja kwenye timu yoyote zaidi ya Simba na huenda wakawa miongoni mwa wachezaji marafiki kama watadumu kwenye timu hiyo muda mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: