Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robo Fainali CAFCL: Simba yapewa Wydad Casablanca

Simba SC Players Kikosi cha Simba

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imerudishwa tena nchini Morocco ambapo katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika imepangwa kucheza na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Wydad Casablanca.

Simba ambaye ametoka kucheza kundi moja na Raja Casablanca ya huko huko Morocco, sasa ataanzia nyumbani katika Dimba la Mkapa na kumalizia nchini Morocco.

Simba SC vs Wydad Casablanca

Al Ahly vs Raja Casablanca

CR Belouizdad vs Mamelodi Sundowns

JS Kabyle vs ES Tunis

Droo ya nusu fainali:

Mshindi kati ya Kabyle na ES Tunis atakutana na mshindi kati ya Al Ahly na Raja Casablanca wakati mshindi kati ya Simba ma Wydad atakutana na mshindi kati ya Belouizdad na Mamelodi Sundowns.

Michezo ya robo fainali itapigwa tarehe 21 na 22 Aprili 2023 na marudiano ni tarehe 28 na 29 Aprili, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: