Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho bado yupo sana Simba, aanika mkakati

Robertinho Sersss Kocha Mkuu wa timu hiyo, Robertinho Oliveira.

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba ambayo imetoka kupata sare ya mabao 2-2 nchini Zambia dhidi ya Power Dynamos, inatarajia kushuka dimbani keshokutwa kuwakaribisha Coastal Union mchezo wa Ligi Kuu Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Uhuru na kutumia mchezo huo kufanyia kazi programu yake mpya.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema ameona mapungufu ya kikosi chake katika kipindi cha kwanza na kufurahishwa na waliocheza kipindi cha pili, hivyo anataingia na mbinu mpya katika mchezo dhidi ya Coastal Union.

Alisema mbinu hiyo ataanza kuifanyia kazi katika mchezo dhidi ya Coastal Union ikiwa ni kipimo cha maandalizi ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos.

“Tumerejea nyumbani kuendelea na programu ya maandalizi ya mechi yetu ijayo, nitakuja na mbinu mpya ambayo nitaanza kuifanyia kazi dhidi ya Coastal Union kwa ajili ya maandalizi yetu ya mechi ijayo ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nimefurahishwa na kipindi cha pili walivyocheza ukiangalia Fabrice Ngoma, Luis Miquissone, Jean Baleke na Saido Ntibazonkiza walicheza vizuri mechi iliyopita, lakini ni muda wa kufanyia kazi changamoto zilizojitokeza Zambia,” alisema Robertinho.

Alisisitiza kuwa anaamini wachezaji wake wote wanauwiano mzuri na atahakikisha anaendelea kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kufikia malengo yao ikiwamo kushinda kila mechi.

Katika hatua nyingine Meneja Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally, alisema bado wanaimani na Kocha Robertinho kuwafikisha katika malengo wanayoyatarajia.

Alisema wanaridhishwa na matokeo wanayoyata uwanjani, lakini bado hawajafikia ile Simba wanayoitaka, na kwamba hakuna ukweli juu ya tetesi zilizopo kuwa kocha huyo amepewa mechi tatu.

“Tunaimani na benchi la ufundi kutufikisha kwenye nchi ya ahadi, tunaridhishwa na kupata matokeo mazuri, lakini bado hatujafikia kuona ile Simba biriani.

“Kwa sasa tunaelekea kwenye soka ambalo tunalitarajia kuliona kwa sababu ya wachezaji wapya kutengeneza muunganiko na wale wa msimu uliopita,” alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: