Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho awaita Mastaa wote Kambini

Chama X Miquissone Mtibwa Robertinho awaita Mastaa wote Kambini

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Robertinho amesema anataka mastaa wote wa Simba kuwa kambini na kuondoka kwenye msafara mmoja kwa lengo la kujenga umoja na mshikamano kikosini.

Kocha Robertinho anapiga hesabu za kupata USHINDI kwenye mechi hiyo ya ugenini kabla ya kurudiana nyumbani wiki ijayo, na tayari amewaita haraka mastaa wote waliokuwa timu za taifa ili wajiunge na wenzao na kupewa mifumo na namna watakavyotakiwa kucheza kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola Zambia.

Chanzo kimesema Clatous Chama alitaka kuisubiri Simba akiwa Zambia, lakini Robertinho amekataa akitakiwa kuwahi kambini Dar kama ilivyo kwa Inonga atakayetua kesho na kuingia moja moja kwenye kambi hiyo iliyopo MO Simba Arena, huku Saido akipata zali la kutakiwa kuungana na timu mjini Ndola kwani anacheza ugenini kesho. Saido atacheza mechi kesho akiwa na Burundi itakayokuwa ikiwania tiketi ya Afcon mbele ya Cameroon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: