Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho atuliza Presha Simba SC

Robertinho Kambini Uturuki.jpeg Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewaondoa presha mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia muda walioupata katika kambi yao nchini Uturuki, umewasaidia kuwajenga.

Ni dhahir kuwa Simba SC wanatambua kwamba ni Young Africans walitwaa taji la ligi msimu wa 222/23 hivyo kocha huyo amewaandaa vizuri wachezaji wa timu huyo kwa ajili ya msimu ujao.

Simba SC itaanza kibarua kwenye mechi za ushindani dhidi ya Singida Fountain Gate kwenye mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii hatua ya Nusu Fainali.

Young Africans waliotwaa taji hilo msimu wa 2022/23 watamenyana na Azam FC Agosti 9 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Robertinho ametoa kauli hiyo baada ya Simba kukamilisha kambi yake nchini Uturuki tayari kwa kuanza msimu wa 2023/24 na tayari wachezaji wapo Dar kwa maandalizi ya Simba Day Agosti 6 2023 Uwanja wa Mkapa.

Robertinho amesema licha ya kupata muda wa wiki tatu ambazo chache kwenye kujenga timu, lakini ameweka sawa kila kitu akishirikiana na wataalamu wengine kwenye benchi la ufundi.

Amesema wasaidizi wake walifanikiwa kumsaidia katika mbinu za kiufundi kwa wachezaji kuelewa haraka kile alichowapa kwenye mazoezi na kuamini kambi hiyo imeleta mapinduzi makubwa.

“Tumefanya kazi mambo mengi katika kipindi hiki, ikiwemo utimamu wa miili, umoja, ushirikiano, mbinu na mifumo tutakayoitumia mara kwa mara katika mechi zetu za ndani na kimataifa, kwa wachezaji kuonekana kuelewa kwa haraka zaidi.

“Nataka kila kitu kimalizike katika muda muafaka ili kuwa tayari kwa msimu mpya, michezo ambayo tumecheza hapa kwa namna kubwa imeweza kutujenga kiasi fulani, uwezo wa wachezaji wapya umeendelea kuimarika, nadhani mashabiki wapunguze presha matumaini yetu ni makubwa sana,” amesema Robertinho

Chanzo: Dar24
Related Articles: