Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho atapona kweli msimu ujao?

Robertinho Kambini Uturuki.jpeg Robertinho atapona kweli msimu ujao?

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Moja ya vitu rahisi sana kwenye soka, ni kumfukuza kocha. Rahisi mno. Wanaweza kukosea wachezaji lakini atakayeondoka kirahisi ni kocha. Wanaweza kukosea viongozi lakini mzigo mzito akatwishwa kocha. Kwa usajili wa Simba msimu ujao.

Kwa presha kubwa ya kushinda mataji waliyonayo, Robertinho akae kwa kutulia. Unapoletewa Jose Luis Miquessone. Unapokuwa na Clatous Chota chama. Watu wanataka ushindi tu. Moja kati ya maeneo muhimu uwanjani ni eneo la kipa.

Simba ilimaliza msimu ikiwa na uhakika kabisa kipa wake namba moja Aishi Manula amefanyiwa oparesheni na atakaa nje kwa muda mrefu. Aliyekuwa kipa wake namba mbili, Beno Kakolanya ameondoka kikosini na kujiunga na Singida Fontain Gate. Kipa pekee wa uhakika waliyebaki naye ni Ally Salim ambaye ni kipa namba tatu.

Naona Simba wanafanya masihara sana na eno hili! Kwangu mimi, kipa ndiye ingekuwa mchezaji wa kwanza kuketwa Kikosini kwa ajili ya msimu ujao. Eneo la kipa ndilo muhimu zaidi kuliko nafasi nyingine zote walizosajili. Hapa ndipo mabao yanapoingilia. Hapa ndipo alama tatu zinapopotelea! Hapa ni mlangoni. Unahitaji kupata mtu wa maana wa kuja kuziba nafasi. Unahitaji mwanaume haswa wa kukupa ubingwa. Wale kina Aubin Kramo, Onana na wengine watakuwa ni kazi bure kama golini kutakuwa na shati.

Taarifa za uhakika ni Jefferson Luiz aliyetambulishwa kama kipa mpya wa Simba kutoka Brazil, afya yake ni longolongo. Simba wanaachana naye! Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson aliwahi kusema “Kipa bora anaweza kukupa alama 15 kwa msimu”. Unajua kwa nini? Ni rahisi tu. Nafasi unazotakiwa kufungwa, yeye ataokoa. Utaondoka na sare au ushindi kabisa.

Eneo la kipa ni muhimu mno uwanjani na ndiyo maana akipatikana wa uhakika, makocha wengi hawana tabia ya kubadilisha mara kwa mara. Simba wamefanya uzembe sana msimu huu. Taarifa za Beno Kakolanya kuondoka walikuwa nazo. Taarifa za Aishi Manula kuwa nje kwa matatibu zote wanazo. Kipa alipaswa kusajiliwa mapema sana. Kinachoendelea kwa sasa ni kama zimamoto tu. Ukitaka kujua umuhimu wa kipa, hata mwamuzi hawezi kuanzisha mechi kama timu haina kipa golini. Nadhani Simba walitakiwa kuwa tayari na makipa wawili wapya kabla hata ya safari ya kwenda Uturuki, mmoja wa nje na mwingine mzawa.

Yule Ally Salim hawezi kuwapa ubingwa kwa sasa. Bado hana ukomavu wa kusimama langoni msimu mzima. Kama wasipopata kipa wa maana, usajili wao wote wa msimu huu utapoteza maana.

Hakuna kitu wanachotaka mashabiki wa Simba zaidi ya kombe. Hakuna. Simba inahitaji kipa wa maana. Baada ya kumkosa Manula Mwishoni mwa msimu uliopita, kila mtu aliona namna timu ilivyoyumba. Hao kina Kramo na Onana, ni kazi bure kama hakuna kipa wa maana. Watu watakuwa wanapigia hata Kibaha, zinaingia kwa Mkapa!

Dirisha la Usajili wa Kimataifa lilifungwa jana na bila shaka yoyote Simba watakuwa walikamilisha usajili wa kipa mpya.

Robertinho atakuwa na kazi kubwa sana msimu ujao. Njia pekee ya yeye kubakia ni kuwapa Simba ubingwa. Kitendo cha kutosajili kipa mapema kinanipa wasiwasi. Mashabiki wa Simba watakuwa wakali sana wasipopata Ubingwa msimu ujao. Mashabiki wa Simba uvumilivu utawashinda. Wanataka kuona mpira mzuri. Wanataka kombe. Kitendo cha kusaini kipa kwa njia ya Zimamoto, kinanipa mashaka makubwa. Kocha Robertinho atapona kweli?

Unahitaji kuwa na kipa bora sana kupata ubingwa. Manula ameifanya Simba kuwa imara sana tangu amejiunga msimu wa sita sasa akitokea Azam FC. Ni Kipa namba moja wa nchi. Amefanya kazi kubwa sana ya kuwalinda mabeki wake. Pamoja na mambo mengine yote, nyuma ya mafanikio ya Simba ndani ya misimu hiyo kuna Manula.

Utawataja kina Chama, Miquessone, ukimaliza wote, weka jina la Manula. Kaokoa nafasi nyingi sana za Simba kufungwa. Kaokoa Alama nyingi sana muhimu kwa timu. Tangu akosekane, Lango la Simba haliko salama. Huwezi kuwa na matumaini ya ubingwa kama hauna kipa madhubuti! Simba walitakiwa kulichukulia jambo hili kwa uzito mkubwa sana.

Jefferson Luiz alitakiwa kuja mapema sana ili Simba wawe na uhakika na afya yake. Najua mchezaji anaweza kuumia muda wowote lakini kama wangekuwepo makipa wawili wa ubora mkubwa, pengine hii zimamoto isingetokea! Timu inayotaka Ubingwa haiwezi kutegemea usajili wa Zimamoto! Manchester United walivyokuwa tu na uhakika wa kuachana na David Degea, fasta wakamleta Andre Onana. Robertinho atapona kweli msimu ujao? Naomba maoni yako kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa namba yangu ya simu hapo juu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: