Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho ashtukia jambo msimbazi

Robertinho Sersss Robertinho ashtukia jambo msimbazi

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kutokana na safu ya ulinzi ya Simba kumpa wakati mgumu kocha mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema ataanza kuwapa nafasi wachezaji wote waliosajiliwa ndani ya kikosi hicho ili waweze kuwa fiti muda wote.

Robertinho alipata wakati mgumu katika michezo ya hivi karibuni baada ya beki wake wa kutumainiwa Henock Inonga kuumia mguu katika mchezo dhidi ya Coastal Union na kukaa nje kwa muda, na nafasi yake ikazibwa na Kennedy Juma.

Kocha huyo anakiri kupata wakati mgumu kwa kuwa alimuamini Inonga kutokana na ubora wake na kuwasahau wengine kama Kennedy na Hussein Kazi ambao nao ni wazuri na ndio maana wamesajiliwa kuitumikia klabu hiyo.

Katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Dar City ambao Simba ilishinda juzi kwa mabao 5-1, Robertinho alianza na mabeki hao lengo ni kuitazama kombinesheni yao ili aweze kuitumia katika michezo ijayo.

“Kila kocha katika timu anakuwa na kikosi cha kwanza ambacho anakitumia mara kwa mara, lakini haisababishi wengine wasipate nafasi. Mimi pia nitaanza kuwapa nafasi Kennedy na Kazi ili na wao wawe tayari kwa mchezo, muda wowote ule waweze kucheza,” alisema na kuongeza kuwa anafurahi kuona Inonga amepona majeraha yaliyomuweka nje.

Katika hatua nyingine Robertinho amewataka wachezaji wake kutokuwa na hofu na wapinzani wao, Al Ahly katika mchezo wa African super League Ijumaa ijayo.

Alisema anafahamu na kutambua ukubwa na wapinzani hao, lakini kitendo cha kila mchezaji atakayepata nafasi kucheza kuwaheshimu itakuwa vyema kufanya vizuri. “Huko nyuma niliona (Simba) walipocheza nao waliwafunga (Ahly), lakini wasiingie na matokeo yale ya zamani kwani mpira unabadilika. Cha msingi ni kupambana dakika zote 90,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: