Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho apangua wawili Simba

Robertinho Sersss Robertinho apangua wawili Simba

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Simba ikiwakabili Prisons dakika chache zijazo, kocha mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliveira 'Robertinho' amefanya mabadiliko ya nyota wawili kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.

Simba ambayo imetoka kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, inahitaji pointi tatu ili kukaa kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu itakapofikisha pointi 12.

Katika kikosi kilichocheza mechi ya marudio dhidi ya Power Dynamos, ni sura mbili tu zilizotamburishwa kuchukua nafasi za wenzao leo kuwakabili 'Wajelajela' katika uwanja wa Sokoine.

Katika kikosi cha leo, amewapumzisha kipa Ayoub Lakred na Jean Baleke walioanza mechi iliyopita walipopata sare ya 1-1 na kuwaanzisha Ally Salim na John Bocco ambaye alitokea benchi na kuonesha kiwango bora dhidi ya Dynamos.

Kikosi hiki hapa

Ally Salim, Kapombe, Hussein, Kened. Che Malone, Mzamir, Ngoma, Chama, Bocco, Ntibazonkiza na Kibu.

Waliopo benchi ni

Ayoub, Isra, Kazi, Kanoute, Hamis, Onana, Chilunda, Baleke na Phiri.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: