Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho amfungia kazi Che Malone

 Che Fondoh Malone.jpeg Che Fondoh Malone

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema baada ya timu yake kuwa na uwezo wa kufunga kila mechi, lakini bado kuna tatizo la mawasiliano katika safu ya ulinzi licha ya Che Malone Fondoh na Kennedy Juma kucheza vizuri. Simba imecheza mechi tano za ligi mpaka sasa, lakini ikiruhusu mabao matatu. . Robertinho amewapongeza wachezaji wake kupata matokeo mazuri na kuiweka timu hiyo kileleni mwa msimamo wa ligi, lakini hafurahii kuendelea kuruhusu mabao licha ya ushindi. Kocha huyo amebaini tatizo katika safu ya ulinzi akisema bado haichezi kwa muunganiko mzuri ikiwa na makosa rahisi ya kujisahau.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tunamtumia Inonga (Henock), lakini sasa hayupo tunawatumia Che Malone na Kennedy. Wanafanya kazi kubwa, lakini tunatakiwa kuwaongezea kitu,” alisema kocha huyo.

“Tunaweza kufunga mabao, lakini tunatakiwa kuongeza umakini na kuimarisha mawasiliano mazuri na mabeki wetu, ili wasiruhusu mabao katika mechi zijazo kwani zitakuwa ni mechi ngumu.”

Robertinho alisema watatumia muda wa mapumziko wa kalenda ya kimataifa kuwaongezea ubora mabeki kabla ya kurudi kwenye mechi zijazo. Hizi siku nitakaa nao ili kuondoa makosa niliyoyaona katika michezo hii ya ligi kwani sikuweza kuwabadilisha kutokana na ratiba ngumu ya mfululizo wa mechi zilizokuwepo. Naamini bado tunaweza kufanya vizuri kabla ya mechi ya Super League dhidi ya Al Ahly na Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: