Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho aimaliza Dynamos

Roberto Robertinho.jpeg Robertinho aimaliza Dynamos

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Simba, Robertinho Oliveira ‘Robertinho’ amewataka wachezaji kuwaheshimu wapinzani wao katika mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos katika Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia, huku akisema ameshawachunguza na kugundua ubora wa wapinzani wao.

Simba inaanzia ugenini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali mara tatu mfululizo na malengo sasa ni kutinga nusu fainali.

Robertinho alisema aliwaona wapinzani wao katika mchezo wa Simba Day kuwa ni moja ya timu nzuri na zinazocheza mpira wa kisasa, hivyo inahitajika kuwaheshimu katika uwanja wao wa nyumbani.

“Mbali ya kucheza nao ila nilijipa muda wa kuwafuatilia zaidi maana ule ulikuwa mchezo wa kirafiki na huu ni wa kimashindano hivyo tunahitaji kupambana kupata matokeo,” alisema.

Kocha huyoa alisema kuwa anatambua uwezo wa kila mchezaji ndani ya kikosi chake na wote ni bora, hivyo atakayepata nafasi ya kucheza ahakikishe anatumia vyema nafasi hiyo kupata matokeo mazuri uwanjani.

“Nawaamini wachezaji wangu wote wana uwezo mkubwa. Nawataka wahakikishe wanapambana na kufanya nilichowaelekeza ili kupata matokeo ambayo yatatufanya kusonga mbele. Hatutakiwi kuwadharau, nimeshawachunguza na kungundua kuwa ni timu bora.

“Nimetumia muda kujaribu kufahamu ni timu ya uwezo gani na tayari nimeshagundua ubora wao uko wapi,” alisema.

Simba wanatarajia kuondoka nchini keshokutwa Alhamisi kwenda Zambia kuwakabili wapinzani wao hao, ikiwa sio mara ya kwanza wekundu kuangukia timu za nchi hiyo kwani waliwahi kupangwa na Nkana na kufanikiwa kuiondosha katika mashindano haya bao la jioni lililofungwa na Clatous Chama pasi ya Hassan Dilunga.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: