Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho aandaa sapraizi ya Phiri

Phiri Robertinho Robertinho aandaa sapraizi ya Phiri

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba jana imeingia rasmi mazoezini kujiandaa kwa ajili ya mechi ya muendelezezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu itakayopigwa kesho Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini benchi la ufundi la chama hilo chini ya kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ linajipanga kutoa bonge la Sapraizi.

Simba iliwasili nchini, Juzi Jumatano ikitokea Misri ilikokwenda kucheza mechi ya marudiano ya African Football League (AFL) dhidi ya wababe wa taifa hilo, Al Ahly na kumalizika kwa sare ya mabao 1-1, hivyo Wekundu wa Msimbazi kuondolewa kwenye michuano hiyo mipya kwa kanuni ya bao la ugenini kwani katika mechi ya awali iliyopopigwa Kwa Mkapa, matokeo yalikuwa 2-2.

Hata hivyo, kiwango ilichokionyesha Simba kwenye mechi mbili na Al Alhy kilikonga nyoyo za wadau wa soka na mashabiki wa klabu hiyo jambo ambalo Robertinho na benchi lake la ufundi wanaamini bado wana maufundi ambayo watu hawajayafaidi na wataanza kuyatoa kwenye mechi na Ihefu.

Robertinho kwa niaba ya benchi la ufundi la Simba alisema kila mchezo huwa na mipango yake na kuna mambo yanaibuka mapya na hali itakuwa hivyo dhidi ya Ihefu kesho.

“Mpango wa Ihefu ni tofauti na ule tulioingia nao dhidi ya Al Ahly lakini lengo ni moja tu, kushinda, alisema Mbrazili huyo ambaye tangu ametua Simba ameiongoza timu hiyo kwenye mechi 16 za ligi bila kupoteza.

Aidha Robertinho aliongeza; “Mfano kuna wachezaji walionyesha ubora mkubwa kwenye mechi zilizopita lakini pia kuna wengine hawakucheza ila sio kwamba ni wagonjwa, hapana ila ni mpango hivyo dhidi ya Ihefu tunaweza kuwashangaza wengi,” alisema.

Licha ya kushindwa kuweka bayana ni sapraizi gani ambayo Simba inaiandaa dhidi ya Ihefu, Mwanaspoti limepenyezewa ni mabadiliko ya kikosi ambapo baadhi ya mastaa huenda wakapumzishwa na kuweka wengine ambao wamekuwa hawajapata muda wa kutosha kucheza kikosini hapo.

Washambuliaji Moses Phiri na Luis Miquissone sambamba na mabeki wa pembeni, Israel Mwenda na David Kameta ‘Duchu’ ni miongoni mwa mastaa wa Simba wanaotarajiwa kucheza mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: