Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Sasa naitaka fainali

Robertinho Kuelekea Robo Robertinho

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kuwa sasa anataka kucheza fainali ya michuano hiyo.

Simba Jumamosi iliyopita ilijihakikishia kufuzu robo baada ya kuwafunga Horoya AC ya nchini Guinea mabao 7-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo umewafanya Simba washike nafasi ya pili katika Kundi C ikiwa na pointi 9 huku Raja Casablanca wakiongoza wakiwa na 13 wote wakicheza michezo mitano.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema kuwa kwanza kabisa anafuraha kubwa ya yeye kufuzu robo fainali, na sasa malengo yake anayaelekeza kufikia fainali.

Robertinho alisema kuwa, hivi sasa anaendelea kukisuka kikosi kitakachokuwa imara na muunganiko mzuri utakaowawezesha kufuzu katika hatua hiyo ya fainali.

Aliongeza kuwa anapata jeuri kutokana na kikosi chake kuimarika zaidi ya kadiri siu zinavyokwenda kwa wachezaji wake kucheza kwa kufauata maelekezo yake na kupata ushindi.

“Kama unakumbuka vizuri, wakati nakabidhiwa niliomba muda wa kutengeneza timu itakayokuwa na muunganiko wa wachezaji watakaokuwa bora.

“Ninashukuru Mungu hivi sasa kila mmoja anaona mabadiliko yaliyokuwepo ya timu, hivi sasa inacheza soka safi la pasi sambamba na kupata ushindi mzuri.

“Hiyo inanifanya nifikirie kufika katika hatua ya fainali ya michuano hii mikubwa Afrika, kwani nina amini ubora wa kila mchezaji wangu nitakayempa nafasi ya kucheza,” alisema Robertinho.

Kikosi cha Simba kinaundwa na wachezaji wengi ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kuipeleka timu robo fainali wakiwemo Clatous Chama, Henock Inonga, Jean Baleke, Aishi Manula, Moses Phiri, Mzamiru Yassin na wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: