Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Nini Yanga? Dawa yao ninayo

Robertinho  Instagram Kocha Roberto Oliveira

Sun, 13 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewapa tano wachezaji wake kwa kupambana kiume na kutinga fainali, kisha akawatumia salamu Yanga, anaokutana nao kwenye fainali itakayopigwa Jumapili akiwataka wajipange kwelikweli siku hiyo.

Akizungumza nasi mara baada ya kuing’oa Singida Fountain Gate kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kwisha kwa suluhu, Robertinho alisema aliwaona Yanga katika mchezo uliopita na Simba itaingia na akili moja tu kusaka taji la kwanza msimu huu.

Robertinho, alisema anawaheshimu Yanga ni timu bora na nzuri, lakini Simba inajua itatokaje kwenye mchezo huo na kwamba watawasimamisha tena wapinzani wao hao.

“Tunakwenda kukutana na Yanga ndio, lakini sikiliza mimi ni kocha ninayependa mechi kubwa kama hizi, huwa napata hisia kubwa pale ninapoona mashabiki wetu wazuri wanafurahia ushindi wetu, tutashinda,”€  alisema Robertinho.

“Itakuwa mechi ngumu, sio mechi rahisi, lakini najivunia sana wachezaji wangu tuna wachezaji wakubwa waliokomaa kucheza mechi kama hizi, nina benchi bora la ufundi ambalo tutarudia tena kushinda mbele yao, lengo letu kuu ni kuchukua hii Ngao.”

Robertinho amepata presha ya kitu kimoja tu cha ubora wa uwanja wa Mkwakwani, lakini akawashusha presha mashabiki wa Simba kwamba ‘Samba’ litakuwepo.

“Wasiwasi wangu ni huu uwanja. Hautupi uhuru kama tunapokuwa tunacheza pale Dar es Saalaam, lakini bado hakuna namna mashabiki wataliona Samba, Simba lazima icheze haitaweza kucheza soka la mipira mirefu,” alisema kocha huyo ambaye huu utakuwa msimu wake wa kwanza kuuanza kutoka mwanzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: