Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Kipa atatua Julai 8

Robertinho Afurahishwa Na Kiwango Simba SC Robertinho: Kipa atatua Julai 8

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba SC, Roberto Oliveira 'Robertinho' amerejea jana, Ijumaa nchini akitokea kwao Brazil ambako alikuwa kwa mapumziko mafupi kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu ujao wa 2023/24.

Vaibu la Kocha Mkuu Robartinho !!! Atua kibabe Uwanja wa Ndege, Afunguka ya moyoni Usajili Simba

Kocha huyo, alitua mwenye tofauti na vile ambavyo ilikuwa ikitarajiwa kuja na kipa raia mwenzake wa Brazil, Caique Luiz Santos ambaye naye anatajwa kumalizana na mabosi wa wekundu hao wa Msimbazi.

Robertinho alieleza kwanini ametua mwenyewe kabla ya kuongelea usajili ambao wamefanya na kile ambacho amelenga kwenye maandalizi yao.

"Atakuja (kipa) kesho kutwa (kesho). Tumefanya usajili wa nguvu ili kuleta uwiano na kuongeza nguvu katika maeneo tofauti, tunajua ubora ambao tulikuwa nao msimu uliopita, tunataka kuwa bora zaidi kulingana na malengo ambayo tupo nayo ili kuvuka vikwazo ambavyo vilitukwamisha,"

"Ufinyu wa kikosi msimu uliopita ulikuwa ukituumiza, tulikuwa na michezo ambayo tulihitaji mabadiliko lakini utofauti wa ubora wa wachezaji ulitufanya kushindwa kupata tulichotaka," amesema na kuongeza;

"Ninafuraha kwakweli na utambulisho wa wachezaji ambao wametambulishwa nilikuwa nikifahamishwa kila hatua kile ambacho kilikuwa kikiendelea, viongozi wamefanya kazi kubwa sasa ni wakati wetu wa kujiandaa na kutafuta uwiano mzuri wa uchezaji kama timu."

Tayari Simba imewatambulisha wachezaji wawili wa kigeni ambao ni Aubin Kramo,27,  kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast na Willy Onana,23,  kutoka Rayon ya Rwanda wote wanauwezo wa kutumika kama mawinga, kushoto na kulia hata ikihitajika wanaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: