Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roberthino awapa maua yao Singida Big Stars

Simba Vs Singida.jpeg Simba ilishinda mabao 2-1 ugenini

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Oliveira Roberto 'Robertinho' amewataka wachezaji wake kutokata tamaa na kuendelea kupambana mwanzo hadi mwisho katika michezo yote ambayo timu hiyo itakutana nayo.

Robertinho kocha mwenye mbwembwe hasa timu yake inapopata matokeo, amesema anaimani kubwa na wachezaji wake wote kwani uwezo wao ndio umewafanya kuwepo hapo.

Amesema mchezo wa jana dhidi ya Singida Big Stars ulikuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa lakini vijana wake walipambana na kuhakikisha wanapata matokeo.

Kocha huyo anabainisha kuwa siyo kazi ndogo kuvuna pointi tatu katika ardhi ya ugenini lakini yote hiyo ni juhudi na umoja wa kila mchezaji katika kufanikisha hilo.

"Ilikuwa mechi ngumu sana, na ikizingatia tulikuwa ugenini, lakini wachezaji wangu mwanzo mwisho hawakukata tamaa hata kidogo ndivyo ninavyotaka,"anasema kocha huyo.

Amesema wapinzani wao walikuwa bora ila wao wakawazidi ndio maana wameondoka na pointi zote tatu.

Robertinho amekuwa na wakati mzuri toka alipojiunga na Simba katika michezo 16 ya ligi ameshinda 14 na kutoa sare miwili huku akiwa hajapoteza hata mmoja.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: