Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Simba kukutana na Power Dynamos CAFCL

Power Dynamos August Power Dynamos

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Power Dynamos ya Zambia ndio itakayocheza dhidi ya Simba katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kupigania nafasi ya kutinga hatua ya makundi.

Simba inafukuzia kutinga hatua hiyo kwa mara ya tano katika mashindano hayo.

Dynamos imetinga hatua hiyo kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ikiwa nyumbani kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndoladhidi dhidi ya African Stars. Matokeo ya jumla ni sare ya mabao 2-2 na Wazambia hao wanabebwa na faida ya bao la ugenini walilopita Namibia walikofungwa mabao 2-1.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Simba itaanzia ugenini kati ya Septemba 15–17 kama ambavyo ratiba ya awali ilikuwa ikionyesha huku ikimalizia nyumbani kati ya Septemba 29 – Oktoba 1.

Awamu ambazo Simba imetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni katika msimu wa 2003, 2018–19, 2020–21 na 2022–23.

Ikumbukwe kuwa Simba iliwafunga mabingwa hao wa Zambia kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki wiki chache zilizopita kwa mabao 2-0 kwenye Tamasha la Simba Day katika Uwanja wa Benjamini Mkapa. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: