Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raja vs Simba... Kisasi cha kitalipwa ugenini?

Bocco Saido Raja vs Simba

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakuna amani kwenye kupoteza hasa baada ya mastaa wa Simba kujichanganya kwenye mchezo wa nyumbani dhidi ya Waarabu, wakapoteza.

Ngoma ya mwisho inatarajiwa kuchezwa Morocco leo Ijumaa, Machi 31, 2023 ikiwa ni mchezo wa kisasi kwa Simba wakiwa ugenini, kazi sio nyepesi kwa timu zote hizi.

Tayari Simba wameanza hesabu kuwania pointi tatu na nguvu katika mchezo huo wa Kundi C kunako Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo inakwenda namna hii:-

KAMBI MAPEMA Machi 24 mastaa wa Simba waliingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ni kete ya mwisho kwenye kundi C.

Wachezaji ambao walianza mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ni pamoja na Jonas Mkude, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, John Bocco, Nassoro Kapama, Moses Phiri, Jean Baleke, Habib Kyombo.

Hawa walikuwa hawajaitwa kwenye timu za taifa ambazo zina mechi za kuwania kufuzu AFCON.

WALINYOOSHWA Mchezo wa pili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-3 Raja Casabalanca.

Katika mchezo huu, Simba walinyooshwa wakiwa nyumbani na mashabiki wao huku bao moja wakitunguliwa kwa penalti.

UGENINI NI NUSUNUSU Mechi mbili ambazo Simba imecheza ugenini imepoteza mchezo mmoja dhidi ya Horoya ikashinda dhidi ya Vipers ya Uganda, hivyo ni nusunusu ndani ya dakika 180.

Haijaambulia sare kwenye mechi za ugenini na wanakwenda kukutana na vinara Raja ambao nao wameshatinga hatua ya robo fainali wakiwa wanaongoza kundi.

WAWILI WACHOMOLEWA KAMBINI Nyota wawili ambao ni mabeki, Kapombe na Tshabalala ambao hawakuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Taifa Stars kilichomenyana na Uganda na kuibuka na ushindi wa 0-1, walichomolewa kambini Simba na kujumuishwa Stars.

Ni kwenye timu ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Uganda ambao ni wa kuwania kufuzu Afcon 2023 Ivory Coast wakipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa ambapo hata hivyo Stars ilipigwa bao 1-0.

KUSEPA KIMAFUNGUMAFUNGU Simba waliondoka nchini Juzi, Jumatano kwa ajili ya kwenda kukamilisha mpango wa mchezo huo na kilifika salama salimin.

MIPANGO KUWAKABILI RAJA IPOJE? “Ukiangalia mpango wa kwanza kutinga robo fainali umetimia na tunakwenda kucheza mchezo wetu wa mwisho ambao nao ni muhimu kwetu.

“Timu tunayokwenda kucheza nayo imetinga hatua ya robo fainali, hivyo nayo ni timu bora, kila kitu kipo sawa na tunaamini tutafanya vizuri.

“Wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa, kikubwa mashabiki wazidi kutuombea na tunawashukuru kwa namna ambavyo wapo pamoja nasi kila hatua.

KAZI IMEKWISHA BAADA YA KUTINGA ROBO FAINALI? “Bado, ndio maana tunakwenda kucheza mchezo wetu huu dhidi ya Raja Casablanca, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kila mchezo ni muhimu, hivyo tunakwenda tukitambua kwamba mchezo huu ni muhimu, ni lazima tucheze kwa umakini,” anamaliza Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: