Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Mwinyi mgeni rasmi Simba vs Al Ahly

Rais Mwinyi Asifu Miaka 59 Ya Muungano .jpeg Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mpaka Sasa taarifa za ndani zinaonyesha kwamba Rais wa Zanzibar, Hussein Ally Mwinyi ndiye mgeni rasmi wa mchezo wa ufunguzi wa African Football League.

Taarifa zinasema Mwinyi atawasili baadaye ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Simba ndio watafungua mashindano hayo wakicheza nyumbani dhidi ya Mabingwa hao wa Afrika Ahly

Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa Mwinyi kuwa mgeni wa heshima kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa tangu awe Rais wa Zanzibar ambapo mara ya kwanza aliwahi kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi mwaka 2023.

Hapa Uwanja wa Mkapa ulinzi ni mkubwa ambapo ukiacha viongozi wakubwa na misafara ya vikosi vya timu mbili hakuna Mt mwingine anayeruhusiwa kupita Geti Kuu la Uwanja wa Mkapa.

Mpaka Sasa bado Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Dk Patrice Motsepe na mwenyeji wao Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia hawajafika uwanjani.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: