Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Power Dynamos kuwakosa mastaa wake muhimu

Lawrence Mulenga Na Dominic Chanda. Lawrence Mulenga na Dominic Chanda.

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa Timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' na Klabu ya Power Dynamos, Lawrence Mulenga huenda akaikosa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba SC ya Tanzania.

Mulenga alipata majeraha makubwa baada ya kugoñgana na Kelvin Kimpamba kwenye Mchezo wa Ligi ya nchi hiyo kati ya Power Dynamos na Zesco United, mchezo uliopigwa Jumapili iliyopita na kutoa sare ya bao 2-2.

Kipa huyo alitolewa na macheka na kuwahishwa hospitali na ambulance kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya haraka.

Aidh, Power Dynamos watamkosa beki wao kisiki, Dominic Chanda ambaye alipata adhabu ya kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Simba, Jean Othos Baleke.

Kwa upande wa Simba wao watamkosa kipa wao Aishi manula ambaye ametoka kwenye majeraha na bado anarejea polepole kwa kufanya mazoezi, winga Aubin Kramo ambaye yupo nje kwa majeraha na beki Henock Inonga mabaye alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union.

Mchezo huo wa marudiano utapigwa Jumapili, Oktoba 1, 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi huku Simba wakiwa na faida baada ya kutoa sare mechi ya awali kwa bao 2-2 wakiwa ugenini kwenye Dimba la Levy Mwanawasa, Ndola Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: