Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phiri aliamsha kambini Simba

Moses Phiri Ctl Phiri aliamsha kambini Simba

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Simba Mzambia, Moses Phiri amesema kuwa sasa malengo ni kuhakikisha anapambana ili arejee katika kikosi cha kwanza cha Mbrazili, Roberto Oliviera.

Mzambia huyo Jumapili alifunga bao lake la kwanza msimu huu wa Ligi Kuu Bara, timu hiyo ilipocheza dhidi ya Dodoma Jiji wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Nyota huyo katika msimu uliopita alipoteza nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na majeraha aliyoyapata katikati ya msimu uliopita.

Akizungumza nasi, Phiri alisema kuwa, anaamini jitihada alizoziweka katika msimu huu ni kupambana apate nafasi ya kucheza katika kikosi hicho cha kwanza cha timu hiyo.

Phiri alisema kuwa, licha ya ushindani uliokuwepo hivi sasa wa wachezaji wapya ambao wamesajiliwa, lakini hiyo haimfanyi yeye aingie katika kikosi cha kwanza katika msimu huu.

Aliongeza kuwa kwa sasa atakachokifanya ni kutumia vema katika kila nafasi atakayoipata kufunga na kuwatengenezea wachezaji wenzake ili afanikishe malengo ya kubeba Ubingwa wa ligi.

“Kwa sasa malengo yangu ni kupambana, kila nitakapopata nafasi ya kucheza kwa kuonyesha ubora wangu wa kufunga mabao ili niingie katika kikosi cha kwanza.

“Ninafahamu ushindani mkubwa uliokuwepo hivi sasa ndani ya timu, nitakachokifanya ni ni kutumia vema kila ninapopewa nafasi ya kucheza kwa kucheza kucheza kwa kujitoa ili nimshawishi mwalimu aendelee kuniamini.

“Haitakuwa kazi nyepesi kwangu bila ya kujibidiisha mazoezini kwa kuonyesha ubora wangu ili kocha anipe nafasi ya kucheza katika timu,” alisema Phiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: