Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Percy Tau: Simba tukutane Misri

Percy Tau Mo Hussein Percy Tau: Simba tukutane Misri

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo wenye hadhi ya ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League (AFL) Simba dhidi ya Al Ahly umemalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Baada ya mchezo huo kocha Mkuu wa Simba Roberto Oliveira amesema ameridhishwa na kile kilichofanywa na wachezaji wake kwenye mchezo huo kwani wameweza kutoka nyuma na kuuchukua mchezo.

Robertinho amesema anaamini chochote kinaweza kutokea katika mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa nchini Misri.

Kwa upande wake kiungo mshambualiaji wa Simba Saido Ntibazonkiza amesema wachezaji wamefanya kila ambacho walipaswa kukifanya na bado wanaaamini wana uwezo wa kuiondosha Al Ahly kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya Vilabu Afrika.

Nyota wa Al Ahly Percy Tau amesema ameridhishwa na matokeo ya mchezo huo kwani Simba walirudi imara zaidi kwenye kipindi cha pili.

Kwa matokeo hayo Simba ili itinge nusu fainali ya AFL inahitaji ushidi wa aina yoyote nchini Misri au sare ya kuanzia mabao matatu.

Vipi nafasi ya Mnyama Simba kusonga nusu fainali ipo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: