Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pale Simba ningebaki na wachezaji 4 tu wa kigeni - Job

Simba Mtihani Mzito Dhidi Ya Jwaneng Galaxy Wikiendi Hii.jpeg Pale Simba ningebaki na wachezaji 4 tu wa kigeni - Job

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka Wasafi FM, George Job amesema kuwa angekuwa kocha katika kikosi hicho basi angebaki na wachezaji wanne tu wa kigeni kati ya wachezaji 12 wanaosajiliwa kwa msimu.

Job amesema hayo akibainisha kuwa wachezaji wengi wa Simba wamechoka na hawana uwezo mkubwa uwanjani hivyo ni vigumu kuipa matokeo timu yao, badala yake wanatakiwa wasajiliwe wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa zaidi.

“Kati ya wachezaji 12 wa kigeni pale Simba ningebakisha wachezaji wanne tu. Ningebaki na Inonga (Henock), Che Malone, Ngoma (Fabrice), na Baleke (Jean) kisha wengine wote ningewaacha,” amesema George Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: