Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Okwa azidi kuivua nguo Simba SC

Nelso Okwa Atemwa Simba Nelson Okwa

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuoneshwa mlango wa kutokea katika Kikosi cha Simba SC, kiungo Nelson Okwa amelalamika kutolipwa stahiki zake mara baada ya kuvunjiwa Mkataba na Klabu ya Simba.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu apewe "Thank You" Okwa ambaye ni raia wa Nigeria anasema;

“Baada ya kuvunja mkataba walisema watanilipa pesa ya kuvunja mkataba lakini bado hadi sasa sijapokea chochote, lakini wamesema wapo kwenye mchakato wa kunilipa, kwa sasa wanipe tiketi ya ndege niondoke nikifika Nigeria kama watanilipa ni sawa,”

Okwa alibakisha Mkataba wa mwaka Mmoja na Klabu ya Simba na muda mwingi alikuwa kwa Mkopo katika Timu ya Ihefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: