Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ONYO: Kama huna tiketi kwa Mkapa usisogee

Muliro Jumanne Marufuku Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewataka watu wote wasiokuwa na tiketi za kuingilia kwenye tamasha la Simba Day siku ya kesho wasijaribu kabisa kuusogolea uwanja wa Benjamin Mkapa, kwani wanaweza kuwa ndiyo chanzo cha tatizo la msongamano.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewataka watu wote wasiokuwa na tiketi za kuingilia kwenye tamasha la Simba Day siku ya kesho wasijaribu kabisa kuusogolea uwanja wa Benjamin Mkapa, kwani wanaweza kuwa ndiyo chanzo cha tatizo la msongamano. Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Jumanne Muliro, na kusisitiza kwamba watakaokiuka watachukuliwa hatua palepale, na kwamba limebaini uwepo wa watu wanaouza tiketi bandia licha ya tiketi zote za tamasha hilo kuuzwa (Sold out).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: