Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa zamani Simba wakosoa 'Thank You' ya Beno

Manula X Beno Kakolanya Beno Kakolanya na Aishi Manula

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba imeendelea kuwapa mkono wa kwaheri nyota wake na juzi ilikuwa zamu wa beki Gadiel Michael, lakini mastaa wa zamani wa timu hiyo wameibuka na kushangazwa na kitendo kilichofanywa na mabosi wa klabu hiyo kumruhusu kipa Beno Kakolanya aondoke kiulaini kwenda Singida FG.

Kalolanya amepewa 'thank you' sambamba na Erasto Nyoni aliyenyakuliwa tayari na Namungo, Victor Akpan, Mohammed Quattara, Augustine Okrah, Jonas Mkude, Gadiel na Nelson Okwa.

Chanzo hicho kinaeleza Bocco alikuwa kwenye mjadala wa kumbakiza ili apewe majukumu mengine lakini wajumbe wengi wameona ni vyema naye akaagwa kama ilivyo kwa wakongwe wenzake kutokana na kiwango chake kwasasa kuonekana kushuka.

"Wapo wengi tu, tunataka kutengeneza timu yenye ushindani mkubwa ili msimu ujao tufanye vizuri, ni kweli timu inahitaji uwepo wa wakongwe lakini hawatusaidii sana, utasajili vipi wakati una idadi kubwa ya wachezaji ambao uwezo wao umeshuka, ni lazima upunguze ili uongeze wengine.

"Unajua ishu ya Bocco ilikuwa ni kubadilishiwa majukumu ila imekuwa ngumu kidogo, sijui kama kutakuwa na mabadiliko mengine ila naye anaachwa," alisema kiongozi huyo.

Hata hivyo wakizungumzia na Mwanaspoti juu ya fagia fagia hiyo, wakongwe wa soka waliowahi kuichezea Simba walisema uamuzi uliofanywa na mabosi hao ni sahihi, ingawa walikosa kwa Kakolanya. Joseph Kaniki 'Golota', mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mtibwa Sugar na Taifa Stars alisema;

"Walichokifanya sio kibaya ila kwa Beno ndiyo wameharibu maana Aishi Manula ameumia na atachukuwa muda mrefu, watasajili kipa mwingine lakini hawajui atamudu vipi ligi yetu."

Kwa upande wa Henry Joseph, kiungo na nahodha wa zamani wa Simba na Stars alisema; "Pengine kuna vitu wameviona kutoka kwa wachezaji hao, hayo ni mabadiliko ya timu na sehemu yoyote yapo, Simba inataka mafanikio na kurudi kwenye ubora wao wa miaka kadhaa iliyopita hivyo ni lazima waondoe wale ambao wanaona kwa wakati huo hawahitaji kuendelea nao.

"Lakini upande wa kipa, sasa wanatakiwa kupata kipa mzoefu ambaye atakuwa tayari kuhimili presha kama ilivyo kwa Djigui Diarra kama nao wataleta kipa wa kigeni, soka letu lina presha kubwa hasa kwa hizi timu za Simba na Yanga, akishindwa kuhimili litakuwa tatizo lingine.

"Hatujui kwanini wameshindwa kumalizana na Beno ila ingekuwa vyema awepo kipindi hiki ambacho Manula anauguza jeraha lake, kwani si rahisi mchezaji atoke kwenye jeraha na kucheza katika ubora ule ule, wakongwe kwenye timu wanatakiwa kuwepo ila inategemea na timu inahitaji nini na wanapata kitu gani kupitia wakongwe hao," alisema Joseph

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: