Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Noti zanusuru watatu Simba

Jimmyson Mwanuke Agoma.jpeg Noti zanusuru watatu Simba

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Usiku Agosti 31, dirisha la usajili wa wachezaji kwa Tanzania lilifungwa huku mastaa watatu wa Simba wakiponea chupuchupu kutolewa kwa mkopo kutokana na kinachoelezwa kuwa ni ishu ya mkwanja.

Awali, Simba ilipanga kuwatoa mshambuliaji Mohamed Mussa, kiraka Jimmyson Mwanuke na kipa Ahmed Feruz, lakini wote wamesalia kikosini baada ya timu zilizowataka kukwama kwenye makubaliano ya mishahara.

Mmoja wa viongozi wa juu wa Simba ameliambia Mwanaspoti kuna mazungumzo yalikuwepo baina ya timu hiyo dhidi ya timu nyingine za Ligi Kuu ili kuwapeleka wachezaji hao kwa mkopo wakapate muda mwingi wa kucheza, lakini wakashindwa kufikia mwafaka kwenye malipo.

“Wamekwama kwenye ishu ya malipo. Ujue Simba inalipa mishahara mikubwa na raundi hii tulitaka timu ikitaka mchezaji wetu kwa mkopo na tukawa tayari kumtoa, basi iweze kumlipa mshahara wake kama sisi tunavyofanya na wengi hapo ndipo wameshindwa hivyo tutakuwa nao na ni muda wao kupambania namba kikosini,” alisema kiongozi huyo.

Mwanuke ambaye msimu huu ni wa tatu kwake akiwa Simba ameshindwa kufurukuta kupata namba mara kwa mara ndani ya kikosi licha ya kubadilishiwa nafasi za kucheza sambamba na Mussa aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea Malindi ya Zanzibar.

Kwa upande wa Feruz aliyeibuliwa kutoka timu za vijana za kikosi hicho, Simba ilitaka kumtoa kwa mkopo ili akapate muda wa kutosha kucheza baada ya chama hilo kuwa na makipa watano hivyo nafasi yake kuwa finyu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: