Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neville: Rashford amefanya kosa kubwa sana

Rashford Vs Ten Hag Marcus Rashford akiwa na Erik Ten Hag

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Gary Neville amesema Marcus Rashford amefanya kosa kubwa kwa kwenda kusherehekea hadharani siku yake ya kuzaliwa wakati timu yake ya Manchester United ikitoka kudhalilishwa na mahasimu wao Manchester City.

Straika huyo Mwingereza alizua sintofahamu kubwa baada ya kupigwa picha akiwa kwenye sherehe ya kutimiza umri wa miaka 26, saa chache baada ya kipigo cha mabao 3-0 nyumbani Old Trafford dhidi ya Man City.

Rashford aliungana na marafiki zake wachache katika mgahawa wa misosi ya kichina kabla ya kuhamishia sherehe kwenye kumbi ya starehe za usiku, kitu ambacho kocha Erik ten Hag alisema “Haikubaliki.” Staa huyo aliwekwa kando kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fulham huko Craven Cottage Jumamosi iliyopita, licha ya kwamba kocha Ten Hag alisema mchezaji huyo alikuwa majeruhi na si ishu ya nidhamu.

Hata hivyo, beki na nahodha wa zamani wa Man United, Neville alisema Rashford alifanya kosa kubwa kwa kufanya alichokifanya wakati timu ikiwa imetoka kupoteza mechi dhidi ya mahasimu wao, Man City. Neville alisema kipindi cha Sir Alex Ferguson hakuna mchezaji angethubutu kufanya kitu kama hicho pindi mnapopoteza mechi.

“Kama tumepocheza mechi, yoyote ile, achana na Manchester derby huwezi kutuona kwenye sherehe kwa wiki moja au mbili. Ukweli sioni kama ni sahihi kuonekana kwenye kumbi za starehe baada ya mechi ya kipigo kwenye Manchester derby. Sidhani kama ni sahihi. Erik ten Hag alisema ni kosa, nataka nisisitize hapo, ni kosa kubwa.”

Chanzo: Dar24
Related Articles: