Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mziki wa Chama wamtisha kipa Jwaneng

Chama X Jwaneng 2 Mziki wa Chama wamtisha kipa Jwaneng

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imetinga hatua ya robo fainali jana kibabe kwa ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana huku kipa wa timu hiyo, Goitseone Phoko akimvulia kofia kiungo wa 'Wekundu hao wa Msimbazi' Mzambia, Clatous Chota Chama.

Kipa huyo amesema kupoteza kwao kwa mabao hayo mtu mbaya kwao ni Chama kwani alikuwa ni injini ya mashambulizi yote makali kwao.

"Ni mchezaji mzuri sana, hata yale mashambulizi mawili yaliyogonga mwamba ni kama bahati kwetu, tangu tunaanza mchezo niliona kwamba ni hatari na sio kwamba hatukujipanga kabla ya mchezo ila tulishindwa kabisa kumdhibiti," amesema Phoko na kuongeza;

"Nadhani tulicheza kwa presha baada ya wapinzani wetu kuanza mchezo kwa kasi sana, unaweza kuona namna ambavyo Chama ni bora akiwa na mipira miguuni kwake hivyo makosa yetu yalikuwa hapo."

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Chama alifunga bao moja huku mengine yakifungwa na Saidi Ntibazonkiza 'Saido', Pa Omar Jobe, Kibu Denis, Ladaki Chasambi na Fabrice Ngoma aliyehitimisha karamu hiyo ya mabao.

Kichapo hicho ni mwendelezo kwa Jwaneng kwani ilikubali pia kichapo cha mabao 4-0, dhidi ya Esperance ya Tunisia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Februari 12, 2022 kisha mechi ya marudiano iliyopigwa Botswana ikachapwa pia 3-0 Machi 19, 2022.

Simba iliyotinga hatua ya robo fainali ya CAF kwa mara ya tano katika kipindi cha miaka sita, ilimaliza nafasi ya pili na pointi tisa sawa na Wydad Casablanca ya Morocco huku Jwaneng Galaxy ya Botswana ikiburuza mkiani na pointi zake nne.

Kinara wa kundi hilo alikuwa ni ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambayo ilikuwa na jumla ya pointi 11 baada ya michezo yake sita.

Katika hatua ya robo fainali Simba inaweza kupangwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Petro de Luanda (Angola) na mabingwa mara 11 wa michuano hiyo, Al Ahly ambazo timu hizo ndizo zilizoibuka kinara wa makundi yao ya 'A', 'C' na 'D'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: