Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzamiru habari nyingine Simba

Mzamiru Goal.jpeg Mzamiru habari nyingine Simba

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa soka, Edo Kumwembe amesema kutokana na aina ya uchezaji wa Mzamiru anaweza kuwa Star Man wa Simba kwenye mchezo wa Wydad dhidi ya Simba utakao pigwa leo saa 4:00 usiku huko Morocco, Casablanca.

“Pambano la kesho (leo) litakuwa la tofauti sana, Simba wamecheza na Raja kule (Casablanca) wakapoteza kwa bao 3, Raja hawakufungua gia kama ambavyo wangeweza kama Kuna kitu wangekuwa wana kihitaji mno.

“Kesho (leo) Wydad watacheza kwa kasi sana na kama Kuna mchezaji ambaye kwa Simba atakuwa Star Man nadhani atakuwa Mzamiru kwa sababu ya tabia yake ya kujituma.

“Kitu cha msingi ni roho ngumu kwa wachezaji wa Simba na kutetea bao lao moja, suala la ushindi sio sana kwa Simba, isipokuwa kulinda walichopata Dar es Salaam,” amesema Kumwembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: