Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwarabu anafia hapa kwa Mkapa

Mohamed El Shenawy Mohamed El Shenawy

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa kwa sasa hapa nchini na Afrika kwa ujumla ni kati ya Simba na Al Ahly inayopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Ijumaa.

Maneno yamekuwa mengi kuhusu mchezo huo kutokana na ubora wa Al Ahly, lakini inaonekana kuwa kama Simba wakiweza kutegua mitego vizuri wanawapasua mabingwa hao wa Afrika kwenye mchezo huo.

Kipa, Al Ahly kwenye michezo yao yote mikubwa wamekuwa wakimtumia kipa Mohamed El Shenawy, ambaye amekuwa na ubora mkubwa, lakini akiwa na UDHAIFA kwenye mipira ya mbali. Kipa huyo amekuwa akifungwa mabao mengi kwenye mashuti ya nje ya 18 hasa yakiwa yanapigwa juu.

Kumbuka bao ambalo Al Ahly walifungwa na Simba ambalo alifunga Luis Misquissone lilikuwa shuti la nje ya 18. Udhaifu huo pia ulionyesha kwenye mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns ambao timu yake ililala kwa mabao 5-2, mawili yote yalikuwa ya nje ya 18, moja lilipigwa juu na lingine chini lakini kumbuka amefungwa mabao ya namna hiyo mara nyingi.

Kama Simba wakitumia udhaifu huo kwa kupiga kutoka mbali wakiwatumia wapigaji wazuri kama Saido Ntibazonkiza, Clatous Chama na Kibu Denis wanaweza kufunga mabao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: