Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimu ni pointi tatu - Robertinho

Chama Robertinho Tu Muhimu pointi tatu - Robertinho

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema pointi tatu ndiyo kitu muhimu zaidi katika mchezo wao wa jana dhidi ya Singida Big Stars ili kuweka matumaini hai ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Big Syats, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Liti, mkoani Singida, jana.

Saido Ntibazonkiza alianza kuiandikia Simba bao la kuongoza dakika ya 26, akimalizia vizuri kazi kubwa iliyofanywa na Denis Kibu lililodumu hadi mapumziko.

Singida ilirudi kwa kasi na kusawazisha kupitia kwa mtokea benchi, Deus Kaseke, ambaye alimalizia kirahisi kazi ya Elvis Rupia, kabla ya Moses Phiri kuingia na kuipa bao muhimu la ushindi.

Kasi ya Singida Big Stars iliongezeka dakika 10 za mwisho ambazo hata hivyo, kikosi cha Robertinho kilikuwa makini kuzima presha hiyo na kuifanya Simba kuwa na ushindi wa michezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu.

Kwa ushindi huo, Simba imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 14, mbili juu ya Aza FC inayoshika nafasi ya pili na Yanga ikiwa ya tatu kwa pointi 12.

Robertinho alisema ulikuwa mchezo mgumu ambao timu yoyote ingeweza kufungwa, lakini ukomavu wa wachezaji wake ulifanikiwa kulinda ushindi.

“Tulijuwa kuwa tutakutana na mchezo mgumu. Singoda Big Stars ina kikosi imara na kimetupa ushindani, nawapongeza wachezaji wangu kwa kuwa walikuwa na kila sababu ya kupigania ushindi.

“Kila mmoja anajua umuhimu wa mchezo huu na kuibuka na ushindi, ndiyo maana kulikuwa na mapambano mengi uwanjani, ambayo yalilenga katika kusaka ushindi.

Tunakwenda kwenye mechi ya kimataifa tukijua kuwa malengo ya ubingwa wa Ligi Kuu yapo hai na tutakuwa kwenye wakati mzuri kujiandaa dhidi ya Al Ahly,” alisema Robertinho.

Akizungumzia kipigo chake, Kocha wa Singida Big Stars, Thabo Senong alisema kikosi chake kilikuwa na mchezo mgumu lakini kuumia kwa mabeki wake wawili, Hamad Waziri na Nicolas Gyan kuliharibu muundo wa ukabaji.

“Ukishakuwa na wachezaji wawili nje, ambao wanakuwa muhimu katika safu ya ulinzi unakuwa matatizoni. Hawa ni wachezaji viongozi na ndiyo maana ilikuwa nafasi kwa Simba kupata bao la pili.

“Lakini hata katika dakika 10 za mwisho tulizoshambulia vizuri, tulikosa utulivu kwani winga wote walikuwa mbali na namba 10 hakuwa karibu na mshambuliaji wa kati,” alisema.

Katika mchezo mwingine wa jana, Tanzania Prisons ilitokea nyuma na kuibuka na ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar wa mabao 3-2.

Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons imejinasua mkiani mwa Ligi Kuu na kusogea hadi nafasi ya 13, huku Coastal ikiwa ya mwisho chini ya Mtibwa Sugar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: