Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msiemtaka kaja! Kibu nje, Onana aanza Simba vs Namungo

Onana Ndani Msiemtaka kaja! Kibu nje, Onana aanza Simba vs Namungo

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji ambaye amekuwa gumzo kwa mashabiki ndani ya kikosi cha Simba Willy Onana amepewa majukumu ya kuimaliza Namungo katika mchezo wa leo.

Simba ni mwenyweji wa Namungo mchezo unaoanza kutimua vumbi saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Onana amekuwa na wakati mbaya apatapo nafasi ndani ya kikosi cha wekundu hao wa msimbazi.

Mbali na Onana Kaimu Kocha wa kikosi hicho Seleman Matola amempa majukumu mlinda mlango Ayoub Lakred ambaye hakupata nafasi katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga.

Katika kikosi cha leo ni wachezaji watatu ndio waliobadilishwa katika kikosi kilichoivaa Yanga na kukubali kichapo cha mabao 5-1

Mshambuliaji tegemeo Kibu Denis hayupo kabisa leo kutokana na majeraha ya enka aliyoyapata mchezo uliopita yaliyosababisha kushindwa kumaliza dakika 90.

KIKOSI KILICHOANZA

SIMBA: Ayoub Lakrade, Shomari Kapombe, Mohammed Hussien 'Tshabalala', Che Malone, Henock Inonga, Mzamiru Yassin, Fabrice Ngoma, Clatous Chama, Jean Baleke, Saido Ntibazonkiza, Willy Onana

NAMUNGO: Jonathan Nahimana, Hassan Kibailo, Emmanuel Asante, Derick Mukombozi, Erasto Nyoni, Hamis Nyenye, Hashim Manyanya, Frank Domayo, Reliants Lusajo, Pius Buswita, Jacob Masawe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: