Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moses Phiri kuongeza kandarasi Simba

Phiri Mbs.jpeg Moses Phiri kuongeza kandarasi Simba

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Simba SC umepanga kumuongezea mkataba mpya, mshambuliaji wao Moses Phiri baada ya kuridhishwa na maendeleo yake na kuwa kwenye mipango ya mwalimu Robertinho.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinadai kuwa, Phiri ambaye ni raia wa Zambia ameridhia kuendelea kusalia klabuni hapo na kwamba huenda akasaini mktaba mpya na muda wowote na itawekwa wazi ni mkataba wa miaka mingapi.

Phiri ambaye alisajiliwa mwanzoni mwa msimu wa 2022/23 alimaliza msimu huo akiwa na mabao 10, lakini alipata majeraha katikati ya msimu ambayo yalimweka nje mpaka mwisho wa msimu.

Msimu huu hajapata nafasi ya kucheza mechi nyingi lakini mpaka sasa ana bao moja alilofunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji.

Hivi karibuni kuliibuka maneno kuwa mchezaji huyo haziivi na kocha Robertinho na ndiyo maana hampi nafasi ya kucheza, lakini yeye na kocha huyo walikanusha tetesi hizo na kusema kuwa wapo shwari wala hakuna tatizo baina yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: