Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwabi avunja ukimya Simba, afichua shida iliopo

Mkwabi Apasua Mkwabi avunja ukimya Simba, afichua shida iliopo

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati hali ya sintofahamu ikiendelea ndani ya Simba ikiwamo kujiuzulu kwa baadhi ya viongozi, Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Swedi Mkwabi amevunja ukimya na kusema kinachoenelea sio sahihi na kuwataka viongozi wote kukaa chini na kumaliza tofauti zao ili kujenga umoja.

Hivi karibuni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba akiwamo mwenyekiti wake, Salim Abdallah ‘Try Again’ walitangaza kujiuzulu, huku viongozi wengine wakifanya mahojiano hali inayodaiwa inawavuruga zaidi wanasimba ambao wana misimu mitatu hawajabeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mkwabi alisema kwa kila mtu kuanza kuzungumza katika mitandao na vyombo vingine vya habari hakuleti suluhisho badala yake kunazidi kuiharibu sifa ya klabu hiyo kongwe jambo linalowapa faida wapinzani na kuwasihi wenzake kulitumia baraza la ushauri ambalo yeye ni mjumbe.

“Kama slogani yetu inavyosema ‘Simba Nguvu Moja’, ningewashauri Wakurugenzi wa Bodi na viongozi kwa ujumla wa Simba kukaa kukaa pamoja chini kutoa tofauti wanazoziona kama watashindwa watumie baraza la ushauri, kwani linaweza kuwaijenga timu kuliko hili kinachoendelea,”

Mkwabi aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Simba Novemba, 2018 kabla ya kujiuzulu Septemba 2019 akiwa amedumu madarakani kwa kipindi kifupi zaidi, hata hivyo alipongeza maamuzi ya baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi walioamua kujiuzulu kwa hiari, hatua aliyosema inaonyesha ukomavu wa uongozi akimtaka mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji kutumia muda huu kuijenga timu bora kwa msimu ujao.

“Hakuna yeyote aliye mkubwa zaidi ya Simba SC kwa kutokufanya vizuri msimu uliopita hatua waliyofikia naona ni maamuzi sahihi na busara, pia tunamshauri Mo Dewji naye atumie muda huu kujipanga upya ili kuitengeneza Simba iliyo bora kwa ajili ya msimu ujao kwani wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba wanawategemea na wamewapa dhamana wao kwa maslahi ya timu,” alisema Mkwabi na kuongeza;

“Kama waliojiuzulu walifanya kwa hiari yao, kuanza kusigana na kusemana katika mitandao sio jambo zuri, Simba tuna Mkutano Mkuu ambao upo kikatiba kama kuna jambo la dharura linalohitaji suluhisho ya haraka uitishwe, lakini kuongea mitandaoni kila mtu kivyake kunaongeza hali ya sintofahamu kwa wapenzi, wanachama na mashabiki.”

Akizungumzia msimu ujao, Mkwabi alisema anaamini kuna uwezekano timu hiyo ikapata mafanikio makubwa zaidi na kufuta maumivu waliyoyapata kwa misimu mitatu mfululizo ukiwamo ulioisha wa 2023/2024 kama tu viongozi watajipanga.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: