Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misimu ambayo Simba ilichukua ubingwa, ilianza hivi hivi - Mchambuzi

Baleke Onana Misimu ambayo Simba ilichukua ubingwa, ilianza hivi hivi - Mchambuzi

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Farhan Kihamu ambaye amesema kuwa klabu ya Simba katika misimu ambayo imechukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ilikuwa ikianza polepole kisha baadaye inachanganya.

Kihamu ambaye ni shabiki wa Simba amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza wa Simba wa Ligi kwa Msimu huu na kuibuka na ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Mtibwa Sugar katika Dimba la Manungu Turiani Morogoro.

Aidha, Kihamu amesema kuwa watu wasishangae kwa Simba kukosa bao katika michezo ya Ngao ya Jamii lakini kwa sasa timu inaanza kuwa imara hivyo wanao uhakika wa kutwaa ubingwa wa Ligi msimu huu.

“Mpira wa miguu ni mchezo wa timu mbili, ili mmoja acheze vizuri ni lazima mwingine awe chini, game ya Kwanza Singida dhidi ya Simba, Singida walikuwa bora sana, game dhidi ya Yanga pia mpinzani alikuwa bora kwenye kila kitu, Simba imeondoka Tanga bila goli zaidi ya penati.

“Ukija kwenye game ya Mtibwa, Mtibwa walikuwa bora kilichotokea ni Simba kutumia vizuri nafasi, mtaani wanasema wameshinda lakini hawana furaha lakini mimi kwangu ukiniambia wameshinda kwangu inatosha, kihistoria Simba hata misimu aliyochukua ubingwa walianza chini sana. This is Simba bwana! Muwa tumeshaukamua," amesema Farhan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: