Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miezi sita ya Chilunda Simba

Shaban Chilunda Magipiessss.jpeg Miezi sita ya Chilunda Simba

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo mshambuliaji, Shaban Chilunda maisha yake Mitaa ya Msimbazi yamefika mwisho baada ya kuachana na timu hiyo kwa kupewa mkono wa kwaheri.

Chilunda ambaye alijiunga na Simba akitokea Azam FC Julai 20, 2023, ametemwa na Mnyama dirisha hili ili kupisha usajili mwingine wa nyota wapya na kushindwa kuonyesha uwezo wake kama alivyotarajia kufanya hivyo akiwa na uzi mweupe na mwekundu.

Ilikuwa ni safari ya maisha ndani ya miezi sita yaliyoambatana na matukio ya kukumbukwa na mwenyewe hataweza kuyasahau alipokuwa Simba. Haya hapa matukio manne yaliyotokea tangu alipotoa Msimbazi.

USAJILI KUSHTUA

Usajili wake ulikuwa ghafla tofauti na majina mengine yaliyotajwa na kuimbwa kila siku 'huyu anaenda huku, huyu anaenda kule'. Chilunda usajili wake ulishtua. Ni jina la sita kwenye usajili uliofanyika Msimbazi katika dirisha kubwa msimu huu.

Hata hivyo, kiungo huyu mshambuliaji aliyewahi kukipiga Hispania katika klabu ya Tenerife akitokea Azam Fc, hakuwa na msimu mzuri Simba na hivyo kuonyeshwa mlango wa kutokea.

DAKIKA 17

Licha ya usajili wake kushtua, hata hivyo, kwenye kikosi cha Simba hakuwa na nafasi na hadi anapewa mkono wa kwa heri, alikuwa amecheza dakika 17 tu. Ni chache. Hata hivyo, licha ya kuwepo mastaa wengine waliocheza dakika chache zaidi wakiwamo Husseni Abeli, Hussein Kazi, lakini uwezo wake ni dakika chache.

Alicheza dhidi ya Tanzania Prisons akipewa dakika moja tu, baada ya kuingia akitokea benchi Simba ikishinda mabao matatu na alicheza tena kwenye mechi dhidi ya Ihefu FC kwa dakika 16 timu yao ikishinda mabao 2-1.

KUPUNGUZA KILO

Hili pia lilikuwa moja ya sababu za kutocheza. Chini ya Kocha Roberto Oliveira 'Robertinho', alikiri alishindwa kupata nafasi kutokana na kuwa na kilo nyingi na kocha huyo alimwambia apunguze.

Chilunda alikuwa na kilo 77 na alipunguza hadi 73 ingawa bado hakupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

PICHA YAKE NA RAIS

Tukio lingine akiwa na Simba na lililomfanya azungumzwe sana licha ya kutokuwa na nafasi ya kucheza, ni lile la picha ya kikosi cha timu hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika picha hiyo wakati wa Tamasha la Simba Day mwaka jana, wachezaji wa Simba walipiga picha ya pamoja na Rais Samia na Chilunda alipata bahati ya kuegemewa na Rais kwenye tukio hilo la kupiga picha wakiwamo wachezaji wa Power Dynamos.

Hii ilisababisha kutazamwa sana kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: