Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda afunguka siri ya kuwatungua Azam

Mgunda Simbaz Mgunda afunguka siri ya kuwatungua Azam

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda amesema kuwa wachezaji wake walimwambia kuwa wanaitaka mechi ya Azam FC ndiyo maana walipambana na kufanikisha kupata ushindi.

Mgunda amesema hayo mara baada ya Simba kuichapa Azam FC mabao 3-0 mchezo wao wa Ligi uliopigwa jana katika Dimba la Mkapa na kuongeza kuwa, Simba sasa imeimarika na kurejesha makali yake.

“Wakati nazungumza nao ilikuwa kama baba na watoto wake. Niliwaambia umhimu wa hii mechi na sio hii tu na mechi nyingine zilizosalia kwenye ligi. Wachezaji wenyewe walisema mwalimu hii mechi tunaitaka, tutajitahidi kadri ya uwezo wetu tupate matokeo, kwa hiyo nawashukuru wao kwa kazi nzuri walioifanya.

“Siku zote nimekuwa nikisema wachezaji wote waliosajiliwa Simba wana haki na wajibu wa kuitumikia timu yao. Katika kazi yoyote kuna haki na wajibu, kwa hiyo wachezaji waliokuwa hawapati nafasi kuwapa nafasi ya kuitumikia Simba wametimiza wajibu wao kuitumikia Simba na kuwatumia wao ni kuwapa haki yao ya msingi kwa sababu lazima wawajibike kwa timu ambayo imewasajili.

“Mashabiki hii ndiyo Simba yao, akama boli limetembea basi tumshukuru Mungu na tujipange kwa ajili ya mchezo ujao,” amesema Mgunda.

Katika msimamo wa Ligi, Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25, Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 56.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: