Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda: Kweli tumefanya makosa, Azam wakatuadhibu

Azam Simba G.jpeg Mgunda: Kweli tumefanya makosa, Azam wakatuadhibu

Mon, 8 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amekiri udhaifu mkubwa uliojitokeza katika safu yao ya ulinzi ambayo yamesababisha kufungwa na Azam FC hapo jana kwenye Dimba la Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Mgunda amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Azam FC, mkoani Mtwara ambapo Azam waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Simba na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo.

“Tunamshukuru Mungu tumemaliza mechi salama na tumepoteza, matokeo sio mazuri lakini ni sehemu ya mchezo. Tumefanya makosa kwa magoli yote mawili tukafungwa, huwezi kumlaumu mtu kwenye soka huwa inatokea.

“Mchezo ulikuwa mgumu na ufundi mwingi sana kutokana na mazingira ya uwanja wenyewe, hivyo tulicheza kwa tahadhari kubwa sana, hayo yameshapita na sasa tunakwenda kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

“Tumejifunza licha ya kufungwa lakini yapo mazuri, kwa hiyo tutakaa benchi zima la ufundi kuona wapi pa kuboresha ili turudi vizuri msimu ujao.

“Ishu ya Ally Salim na makosa aliyofanya uwanjani hayo ni mapungufu ambayo tunakwenda kuyafanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi. Lakini tukumbuke kuna mangapi mazuri yamefanyika pia.

“Hata sisi tunataka matokeo mazuri, ni kweli inauma lakini niwaambie mashabiki wa Simba kwamba tumeumia sote, kikubwa ni kwenda kujipanga na kuona namna ya kufanya vizuri mechi zijazo,” amesema Mgunda.

Mpaka sasa unaweza kusema Simba imekosa mataji yote msimu huu, kwani wametolewa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye hatua ya robo fainali, Kombe la Shirikisho la Azam wametolewa, ngao ya jamii wamekosa, Mapinduzi Cup wamekosa n ahata ubingwa wa Ligi, Yanga ndiyo inaonongoza huku ikihitaji mchezo mmoja tu kutangaza ubingwa kati ya mitatu iliyosalia kutamatika kwa ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: